Kupakua nyaraka za TESSA kutoka kwenye tovuti

 Kwa Kompyuta zinazotumia Windows XP au matoleo ya sasa.
(Tafadhali zingatia hili, kama kompyuta uliyonayo inatumia matoleo ya zamani ya Windows, unaweza usifanikiwe kupakua nyaraka za TESSA au mchakato unaweza kuwa tofauti.)

Hatua 1: Pakua folda lenye zipu na kuweka kwenye diski kuu ya kompyuta yako ya mezani au ya mkononi
Ili kupakua nyaraka, bofya “hapa” kupakua majalada.
(Jalada hili ni kubwa sana, kwa hiyo linaweza kuchukua muda mrefu kufunguka).

Hatua 2: Chagua ‘Akibisha’ ili kuhifadhi majalada kwenye diski kuu yako.
(ukifanikiwa kuchagua, akibisha majalada hayo kwenye eneo kazi (desktop) la kompyuta yako au andika kumbukumbu ya mahali ulipoliakibisha)

Hatua 3: Kuchota majalada kutoka kwenye folda la zipu.
Baada ya kuwa umepakua folda na kuliweka kwenye kompyuta yako, bofya kulia folda lako na teua ‘Chota yote’ au ‘WinZip’ kutoka kwenye menyu. Yachote na kuyahifadhi majalada mahali unapotaka kuyahifadhi kwenye kompyuta yako.

Hatua 4: Kufungua majalada uliyoyapakua
Nyaraka hizi sasa zimeakibishwa kwenye kompyuta yako ya mezani au ya mkononi kwenye folda ulilolichagua. Ili kuziona nyaraka hizi bofya folda linaloitwa ‘cd_temp’.
Fungua waraka unaoitwa ‘unisome’ ulioakibishwa kwenye folda hii. Huu utakueleza namna ya kufungua nyaraka za TESSA ulizozipakua.
Sasa unaweza kunakili nyaraka hizi kwenye kinyonyi chako au kwenye Sidii ROM (soma maelekezo hapa chini).

Kuakibisha majalada kwenye Sidii.
(Tafadhali fahamu kwamba majalada mengi ya nchi mbalimbali yana ukubwa wa kati ya 300-500 MB, kwa hiyo hakikisha kwamba Sidii yako ina ukubwa huo au zaidi ili kuweza kutunza majalada yote).

Hatua 1:
Bofya kulia folda la nyaraka ulizopakua na kuzichota. Teua ‘Tuma kwenye’ kisha ’Kiendeshi cha Dividii/Sidii’.

Hatua 2:
Fungua folda la kwenye Kiendeshi cha Dividii/Sidii na unapaswa sasa kuona majalada yanayosubiri kuandikwa kwenye Sidii.
Teua ‘Andika majalada kwenye Sidii’ kutoka kwenye menyu ya kushoto na Sidii ya Kuandikia itaonekana.

Hatua 3:
Fuata hatua za kuandika kwenye Sidii na mara tu unapoanza, weka Sidii tupu kwenye kompyuta yako ya mezani au ya mkononi.
Mara tu mchakato wa kuandika majalada kwenye Sidii unapokamilika, itoe Sidii. Inapaswa sasa kuwa na nyaraka zote za TESSA kutoka kwenye tovuti.

Kuakibisha majalada kwenye kinyonyi (USB).
Majalada haya yanaweza pia kuakibishwa kwenye kinyonyi. Tafadhali fahamu kwamba majalada mengi ya nchi mbalimbali yana ukubwa wa kati ya 300-500 MB, kwa hiyo hakikisha kwamba kinyonyi chako kina ukubwa huo au zaidi ili kuweza kutunza majalada yote.